fB insta twitter

Alichokiandika Samatta baada ya ushindi wa Yanga wa 5-1 Comoro

on

Ushindi wa 5-1 wa Yanga katika mchezo wao wa kwanza wa round ya kwanza wa Club Bingwa Afrika dhidi ya N’gaya Club ya Comoro, umekuwa stori na kufanya kila shabiki wa soka la Bongo kufurahia kuona Tanzania ikiwakilishwa Comoro ambapo watarudiana baada ya wiki moja Dar es Salaam.

Mitandao ya kijamii kwa upande wa soka walikuwa wakiijadili ushindi huo ambao kama Yanga wakifanikiwa kuifunga N’gaya au kutoka sare yoyote ile watasonga mbele round inayofuata katika michuano hiyo, ambapo Yanga ndio timu pekee ya Tanzania bara inayoshiriki.

Kufuatia ushindi huo mtanzania Mbwana Samatta alitumia ukurasa wake wa twitter kuandika ujumbe wa kuipongeza Yanga, Samatta ameonesha uzalendo na kufurahia ushindi huo kwa kuandika “1-5 safi sana,waambieni kabisa bongo kuna 7 zinawangoja yanga African”

VIDEO: Yanga vs Azam FC January 7 2017, Full Time 0-4

Soma na hizi

Tupia Comments