Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali leo June 16, 2017 imetoa zawadi kwa Wanafunzi bora wa masomo ya Kemia na Biolojia wa Vidato vya Tano na Sita katika sherehe fupi ya kila mwaka yenye lengo la kuhamasisha vijana kupenda masomo ya Sayansi.
Mkemia Mkuu Samweli Manyele amesema kuwa sherehe hiyo hufanywa kila mwaka ili kuwahamasisha wanafunzi kupenda masomo ya Sayansi huku akielezea kazi zinazofanywa na Ofisi yake ikiwa ni pamoja na uchunguzi wa kimaabara na kufanya uchunguzi wa vielelezo vya makosa ya jinai na DNA.
>>>“Tulikuwa na sherehe fupi kwenye Viwanja vya Ofisi ya Mkea Mkuu wa Serikali ili kutoa zawadi kwa wanafunzi bora wa somo la Kemia na Biolojia kwa Kidato cha Tano na cha Sita, kwa wavulana na wasichana kwenye kila somo. Kila mwaka na hii sherehe tunaifanya kila mwaka ili kuwahamasisha wanafunzi wapende masomo ya Sayansi.” – Samweli Manyele.
GUMZO JIPYA: Baada ya Vyeti, Mhandisi FAKE akamatwa Mwanza