AyoTV

VIDEO: Mbunge Jumaa Aweso katusogezea changamoto iliyowaondoa wabunge wawili Pangani Tanga

on

Inawezekana suala la miundombinu ya barabara katika baadhi ya maeneo ikawa ni tatizo kubwa hapa nchini, sio ajabu leo mbunge wa Pangani-Tanga Jumaa Aweso anaposema anatamani hata fungu lake la mshahara lingetosha basi angelimaliza kabisa tatizo hilo jimboni kwake kwakuwa ni tatizo ambalo limesababisha hata wabunge wawili waliomtangulia kupigwa chini kwa sababu ya tatizo hilo.

Changamoto kubwa katika wilaya ya Pangani ni suala la barabara ya Pangani-Sadani, hili limekuwa ni tatizo la muda mrefu ambalo limeshasababisha hata wabunge wawili walionitangulia kupigwa chini kwasababu hiyohiyo ya barabara‘ –Jumaa Aweso

Hii imesababisha mateso na kuvunja imani kwa wananchi wa Pangani, niiombe serikali kwamba tumeshafanya upembuzi hivyo itujengaa barabara ili tuweze kuinua uchumi kulingana na fursa zilizopo Pangani‘ –Jumaa Aweso

Laiti kama mshahara wangu ungeweza kujenga barabara ya Tanga-Pangani basi ningeusamehe ili kuhakikisha hili linatekelezeka, lakini naamini Rais Magufuli ataliona hili ili tuweze kuinua uchumi kwa wananchi wetu‘ –Jumaa Aweso

Unaweza kuendelea kumsikiliza hapa mbunge Jumaa Aweso katika exclusive interview na Ayo TV

ULIIKOSA HII MBUNGE JUMAA AWESO KUHUSU TATIZO LA MAJI PANGANI

Soma na hizi

Tupia Comments