Bado burudani ya soka ipo Zanzibar kwa kuendelea kuchezwa michezo ya Kombe la Mapinduzi, baada ya kupigwa mchezo wa tatu wa Kundi B mchana wa January 5 kwa kuzikutanisha timu za Mafunzo ya Zanzibar na Mtibwa Sugar ya Morogoro na mchezo kumalizika kwa Mtibwa kuibuka na ushindi wa goli 1-0.
Usiku wa January 5 ulichezwa mchezo wa nne wa Kundi B kwa kuzikutanisha timu za Azam FC dhidi ya Yanga ambapo timu hizo zote zinachuana kwa karibu kutaka nafasi ya kuongoza katika Ligi Kuu Tanzania Bara, ila kisasi kikahamia katika mchezo wa Kombe la Mapinduzi, haukuwa rahisi na ulikuwa wa kukamia kwa nahodha wa Azam FC John Bocco na beki wa Yanga Kelvin Yondani, kitendo ambacho kilipelekea John Bocco kuoneshwa kadi nyekundu.
Hata hivyo mchezo huo ulimalizika kwa sare ya goli 1-1, baada ya Azam FC kufunga goli la uongozi kupitia kwa Kipre Tchetche dakika ya 58, Yanga walikuja juu na kuongeza mashambulizi ila mabadiliko ya kuingia kwa beki wake wa kimataifa wa Togo Vicent Bossou kulizaa matunda baada kufanikiwa kuisawazishia Yanga goli dakika ya 83.
Sare hiyo imeenda kubadilisha msimamo wa Kundi B, sasa Yanga atakuwa kileleni kwa tofauti ya magoli akiwa na point 4, akifuatiwa na Mtibwa Sugar wenye point nne, Azam FC wenye point 2 na Mafunzo wakishika mkia kwa kuwa hawana point hata moja, Azam FC atacheza mchezo wake wa mwisho dhidi ya Mafunzo na Yanga dhidi ya Mtibwa Sugar.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyezahapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE