Siku moja tu baada ya Waziri wa Mwigulu Nchemba kuwasimamisha baadhi ya watumishi kwa ubadhirifu huko Pwani, headlines zimerudi tena katika Wizara ya Maliasili na utalii baada ya Waziri Prof. Jumanne Maghembe kuwasimamisha maofisa misitu.
Waziri Maghembe leo ametangaza kumsimamisha kazi Mkurugenzi wa mipango na matumizi endelevu ya rasilimali za Misitu Mohamed Kilongo na maofisa wa misitu katika Mikoa yote nchini ili kupisha uchunguzi wa upotevu wa mapato ya Serikali.
Waziri Maghembe amesema agizo hilo limekuja kutokana na ubadhirifu wa ukusanyaji wa maduhuri ya Serikali yanayotokana na rasilimali za misitu kutoka katika Mikoa na Wilaya kwa kutowasilishwa kwenye mfuko mkuu wa Serikali.
Pia amewataka maofisa hao watumie muda wa siku 10 kuanzia leo kuhakikisha maduhuri yote yaliyokusanywa yanapelekwa benki pamoja na kukusanya vitabu vya mapato kinyume na hapo watachukuliwa hatua kali.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyezahapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.