Michezo

Kauli nzito ya Zlatan kwa wakongwe wa Man United wanaomkosoa Pogba

on

Mshambualiaji wa zamani wa club ya Man United anayecheza LA Galaxy ya Marekani kwa sasa Zlatan Ibrahimovic amewakosoa wachezaji wakongwe wa zamani wa Man United kwa madai ya kuwa hawakupenda Paul Pogba ahame 2012 na kurudi tena na mara nyingi wakiwa kwenye kazi zao wamekuwa wakimkosoa, Zlatan ambaye amewaita wachezaji hao kwa jina moja la ‘Class of 92’

“Hawachezi tena pale (Man United)n wapo kwenye TV na wanalalamika muda wote kwa sababu hawapo tena katika timu, kama unataka kwenda kufanya kazi katika club nenda katafute hiyo kazi, Pogba alikuwa Man United wakati anachipukia halafu alihama na baadae akarudi tena katika utawala wa Ferguson hakuwa anapenda hilo ndio maana hawakuwahi kumuhama Ferguson”>>>Zlatan

Garry Neville

“Walikuwa hata hawaongea kama Ferguson anakuwa hajawaruhusu kufungua vinywa, hivyo kwa sasa ninavyowaona wanaongea sijui kama Ferguson kawaruhusu au la”>>>Zlatan Ibrahimovic

Kundi la Class of 92 linawajumuisha wachezaji wa zamani wa Man United kama Garry Neville, Paul Scholes, Nicky Butt, Phil Neville na Ryan Giggs kwamba walikuwa hawaongeiongei chini ya Sir Alex Ferguson kwa sasa lakini wamekuwa wakimkosoa sana Paul Pogba ambaye alizua gumzo baada ya kupost picha flani hivi iliyokuwa inahisiwa kuwa ni anafurahia Jose Mourinho kufukuzwa kazi ndani ya Man United huku Neville akiwa kinara.

Mashabiki wa Simba na Yanga waiongelea Simba VS AS Vita hapo kesho !!

Soma na hizi

Tupia Comments