Waandamanaji katika Mji wa Beirut wamekabiliana na vikosi vya usalama vya Lebanon wakiipinga Serikali.
Maafisa wa usalama walirusha mabomu ya machozi kwa kundi la waandamanaji waliokuwa karibu na bunge.
Waandamanaji hao walikasirishwa na mlipuko uliotokea Jumanne, ambapo maafisa wanasema ulisababishwa na tani 2,750 za kemikali ya ammonium nitrate ambazo zimekuwa zikihifadhiwa kwa njia isiyo sahihi tangu mwaka 2013.
Raia wengi wa Lebanon wanasema upuuzaji wa serikali ndio chanzo cha mlipuko huo, uliosababisha vifo vya watu karibu 137 na kujeruhi wengine 5,000.