Polisi katika kaunti ya Kericho nchini Kenya wanamshikilia Mwanaume mmoja mwenye umri wa miaka 57 kwa tuhuma za kumuua na kisha kumfukia Mtoto wake mwenye umri wa miaka 25 baada ya wote wawili kulewa na kuanza kugombana.
Polisi wanasema wawili hao walifika nyumbani kutoka Bar ambako walikuwa wakilewa pombe, walipofika nyumbani wakaanza kugombana, Baba akampiga Mtoto wake na kifaa butu kichwani na alipobaini amefariki akamfukia kwenye shimo.
Polisi wanasubiri amri ya Mahakama kufukua mwili wa Marehemu kwa ajili ya uchunguzi zaidi huku Mtuhumiwa akisubiri kufikishwa Mahakamani.