Kuelekea fainali ya tuzo za mchezaji bora wa dunia kwa mwaka 2015 zitakazofanyika Zurich Uswiss January 11 2016, naomba nikusogezee mafanikio ya washindani wa jadi wa tuzo hizo. Kwa mwaka 2015 wachezaji watatu waliofanikiwa kuingia katika fainali ya tuzo hizo ni Messi, Neymar na Ronaldo. Kwa kiasi kikubwa washindani wakuu ni Messi na Ronaldo hao ndio washindani wenye nguvu kwa tuzo ila haya ndio mafanikio ya kila mmoja kwa mwaka 2015.
4- Cristiano Ronaldo yeye anatajwa kushinda tuzo binafsi zaidi ya Lionel Messi ambaye kwenye msimu wa 2014/2015 amefanikiwa kushinda taji la Super Cup na Klabu Bingwa dunia, lakini Ronaldo amefanikiwa kutwaa tuzo ya FIFA Ballon d’Or na European Golden boot.
3- Kwa timu ya taifa na vilabu
Lionel Messi amefanikiwa .ufunga magoli 52, assist 26 katika michezo 62 aliyocheza kwa FC Barcelona na timu yake ya taifa ya Argentina. Lakini kwa upande wa Cristiano Ronaldo ameshinda magoli 57, assist 18 katika michezo 58 kwa timu yake ya taifa ya Ureno na klabu ya Real Madrid.
2- Mafanikio yao kwa ngazi ya vilabu vyao (FC Barcelona na Real Madrid)
Lionel Messi amefunga magoli jumla ya magoli 48 kwa michezo yote ya FC Barcelona aliyocheza kwa mashindano yote kwa mwaka 2015, lakini ametoa assist 23 katika michezo 54. Wakati Cristiano Ronaldo amefunga jumla ya magoli 54, assist 18 katika michezo 53 akiwa na Real Madrid kwa mwaka 2015.
1- Kwa timu zao za taifa Ronaldo na Messi (Argentina na Ureno)
Lionel Messi amefunga goli 4, assist 3 katika michezo 8 ya timu yake ya taifa ya Argentina, wakati Cristiano Ronaldo amefunga jumla ya magoli matatu katika michezo katika mechi 5 alizocheza na hajatoa assist yoyote.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyezahapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.