Mshambuliaji wa Liverpool aliyejiunga na AC Milan kwa mkopo Mario Balotelli, ameendelea kufurahia maisha ya kurejea katika klabu ya AC Milan baada ya kuondoka klabuni hapo kwa msimu mmoja, Balotelli akiwa na rafiki yake Antony Uberti walipiga picha wakiwa katika helicopter.
Baada ya kumaliza msimu bila mafanikio na klabu ya Liverpool, Balotelli hakuwa sehemu ya kikosi cha Italia kinachonolewa na kocha Antonio Conte katika mechi dhidi ya Bulgaria iliyochezwa Septemba 6 na Italia kuibuka na ushindi wa goli 1-0.
Awali kocha wa klabu ya AC Milan ya Italia Sinisa Mihajlovic aliwahi kunukuliwa na vyombo vya habari kuwa Balotelli ameongezeka uzito, Balotelli pamoja na rafiki yake Antony Uberti walipiga picha katika pozi tofauti tofauti wakiwa milimani, hii ikiwa ni sehemu ya mapumziko ya mechi za kimataifa.
PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia za siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos