Pichaz za maeneo mengine alikofika Rais Obama kwenye nchi 50 alizotembelea…
Share
3 Min Read
SHARE
Safari ya Rais Obamandani ya Kenya imeweka rekodi ambayo sikuwa nafahamu, kumbe kwa kipindi ambacho Rais Obamaamekaa madarakani ambacho ni kama miaka saba hivi anakuwa ametembelea jumla ya nchi 50 nje ya Marekani.
Mmoja ya Wapigapicha wa White House, Pete Souza kazitoa picha 50 ambazo hazikuwahi kuonekana mahali popote !!
Hapa ziko pichaz 12 kati ya hizo mtu wangu.
Aliwahi kufika Msikiti wa Istiqlal uliopo Jakarta, Indonesia… Katikati yukoImam Ali Mustafa Yaqub, na pembeni mwenye suti na kilemba ni Michelle Obama… November 2010 alikuwa kwenye Msikiti huo na alifuata taratibu za hapo kwa kuvua viatu yeye pamoja na mkewe.Kuna wakati alijiachia bila Timu ya Walinzi wake, hii alikuwa anakatisha zakePanama Marekani, April 2015.Wakati mwingine anaenjoy story na watu wa kawaida kabisa, hapa alikuwa anapiga story na Mkuu wa Wafanyakazi wa Mgahawa wa Esperanza uliopo San Jose del Cabo, Mexico. Hii ilikuwa June 2012.Hapa alitembelea Sanamu ya Yesu iliyoko Rio De Janeiro, Brazil March 20, 2011.Kwenye safari zake alifika na Egypt pia, akatembelea Mapiramidi ambayo nayo yamo kwenye maajabu ya Duniani.. Hii ilikuwa June 2009.Aliwahi fika China pia November 2009. Hapa alikuwa kwenye ukuta mkubwa ambao uko pia kwenye Maajabu ya Dunia, ‘the Great Wall of China’.Muda mwingine wanakuwa na Stori kwenye mazingira tofauti kabisa na Office, hapa alikuwa na Chancellor wa Ujerumani, Angela Merkel.. Hii ilikuwa Ujerumani June 2015.Ishu ya kudance ni kawaida tu kwake, hapa alikuwa na Wanafunzi wa Mumbai, India November 2010.. Pembeni ni mkewe,Michelle Obama.November 2010 aliwahi kufika Kamakura, Japan.. Moja ya vitu alivyoenjoy ni kula Ice Cream !! Alitembelea pia haya maeneo ya Kihistoria kwenye nchi ya Burma, utamaduni wao inabidi uwe pekupeku bila viatu.. alivua pia, hii ilikuwa November 2012.Hapa ni ndani ya Gereza lililopo Visiwa vya Robben, Cape Town South Africa… Hiki ndio chumba alichowahi kufungwa Hayati Nelson Mandela.. Hii ilikuwa June 2013.Rais Obamaalitembelea pia Maeneo ya Makumbusho ya Stonehenge yaliyopo Wiltshire, England… Hii picha imepigwa Sept 2014.
Nitakutumia stori zote ukibonyeza hapa>>> TwitterInstaFBna nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videosili kila video ya AyoTV ikufikie.