Mwimbaji wa Bongofleva Baraka The Prince ameonesha kusikitishwa na kifo cha aliyekuwa Waziri wa Katiba na Sheria Balozi Agustine Mahiga aliyefariki asubuhi ya leo huko Dodoma.
Baraka ameandika haya…>>>>Duuh Katika Siku Nimeamka Nayo Vibaya ni hii Ya Leo Kifo Kifo Kifo 😭😭😭😭 🙌🏿🙌🏿,Mzee wangu Nitaishi katika Busara Zako Ulizowahi kuniachia”Nimeshtushwa Sana Huu msiba Jaman,Nakumbuka Mara Ya kwanza.
Nakutana Na mzee wangu Dr.Mahiga Ilikuwa Dodoma Moja Kati Restaurant Ya Hotel Flani Dodoma Nilikua Nikipata Dinner,Mzee Mahiga Kwa Hekma Na Busara Zake Alivyoniona Akutaka Kuvunga Au kuficha Furaha Yake Alinialika Tujumuike Wote Katika Meza Yake.
Nami Sikusita Nikasogea Katika Meza Yake Cha kwanza Akaniambia Yeye sio shabiki sana wa Miziki Ya Kidunia Kwa maana Ya BONGOFLAVA Lakini Yeye Ni Shabiki Mkubwa Wa Mziki Wangu Kwakua Huwa Ninaimba Mziki Tulivu Na Wenye Maadili,Nilifurahi Sana na Ilifanya Siku Yangu Kuisha Poa sana.
Tulipata Dinner Pamoja Na Kwa mda mchache Tu Niliokaa Nae Nilijifunza Mengi Sana Kutoka Kwa Mwana Diplomatic Huyu Na Nilichukua Mengi Sana Ya kunijenga Kiakili na Kuyajua Maisha Ni wapi Yalipo Na Yanapoelekea.
Kikubwa Na kumbuka Aliniambia Barakah Kijana wangu Mafanikio Ya kweli Yapo Mbali sana Na katika Maisha Yako Usipende Shortcut Way Hata kama Utafanikiwa Ila Mafanikio Yako Hayotokuwa Imara Na Yakudumu,Jenga Misingi Iliyo Imara Ili Utapofanikiwa Usije Kupoteza Mafanikio Yako,1.Jiamini kwa kila unachokifanya 2.Mtu Asikuaminishe Bila Yeye Huwezi 3.Simamia Kile Unachokiamini Kinaweza Kukupa Mafanikio Na usije kuyumbishwa Hata kidogo 😭😭😭😭.
Daah Haya maneno Nitaishi Nayo Leo Kesho mpaka mwisho Wa Maisha Yangu,Mzee Nilitamani sana Siku moja Uje Kuyaona Mafanikio yangu Kwa Ukubwa Ambao Allah Kanipangia Ila Umetangulia Ghaiiii,Tangulia Baba Tutaonana Siku moja tena…Rest In Paradise Father Dr.Mahiga 😭😭🙏🏿