FC Barcelona leo katika uwanja wao wa Nou Camp waliwakaribisha Granada kucheza mchezo wao wa 33 wa Ligi Kuu ya Hispania na kupoteza game hiyo kwa magoli 2-1.
Pamoja na kuwa Barcelona walioata goli la mapema la uongozi dakika ya 23 kupitia kwa Lionel Messi, Granada wao walifanikiwa kurudi mchezo kwa magoli ya Darwin Marchis dakika ya 63 na Jorge Molina dakika ya 79.
Kipigo hicho kinaiweka pabaya Barcelona katika mbio za kuwania Ubingwa kwani sasa wameshuka hadi nafasi ya tatu LaLiga wakiwa na point 71 sawa na Real Madrid waliopo nafasi ua pili kwa tofauti ya magoli, huku Atletico Madrid wakiongoza kwa point 73.
Kama Barcelona angeshinda mchezo wa leo basi angeongoza Ligi kwa kuwa na point 74 na kujiwekea nafasi ya kutwaa Ubingwa wa LaLiga 2020/2021 ila kwa sasa timu nne zote za juu zina nafasi ya kutwaa Ubingwa wa LaLiga hadi Sevilla aliye nafasi ya nne kwa kuwa na point 70 ikiwa imesalia michezo mitano LaLiga kumalizika.