Ugumu wa maisha unaongeza ubunifu, ubunifu mwingine unakuweka pabaya.. huu wa huyu jamaa sidhani kama tunaweza kuuita ni ubunifu ila jamaa aliamua tu atumie njia hii ili apate tu njia ya kupata mkate wa siku.
Mmiliki wa Bar ya Siaya, Kenya alimshtukia jinsia ya mmoja ya wahudumu wake wa Bar kwamba jinsia yake sio ya kike.. Akatoa taarifa Polisi kuhusu mhudumu huyo, walipokuja kumpekua jamaa alijitetea kwamba ana jinsia mbili.
Jamaa huyo anaitwa Michael Obiero alikamatwa baada ya kufanya kazi kwa siku mbili kwenye Bar hiyo akijitambulisha kwa jina la Brenda na pia alikuwa akilala chumba kimoja na wahudumu wengine wa kike.
Polisi walimlazimisha avue nguo zake ili wamkague, wakaona hakuwa na muonekano wa jinsia ya kike, wanaendelea na upelelezi ili kujua ukweli japo Mkuu wa Polisi Kaunti ya Bondo amesema hata mmiliki wa Bar hiyo huenda akawa na makosa ya kumuajiri jamaa huyo bila kumkagua.
Ni halali yako kupata kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>> twitter Insta Facebook