Mwenyekiti wa Chama cha Tanzania Labour Party (TLP ) Augustine Mrema amezungumza na waandishi wa habari pamoja na mambo mengine ameitaka Serikali ya nchi hiyo inayoongozwa na Rais John Magufuli kumlipa Sh2 Bilioni kama fidia ya kesi alizowahi kusingiziwa katika utawala wa awamu ya tatu.