Mbunge wa Kigoma Mjini na Kiongozi wa Chama cha ACT-wazalendo, Zitto Kabwe amesema kuwa amemuandikia barua Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli kuhusu janga la virusi vya Corona linalosambaa duniani hivi sasa.
Akisoma na kufafanua ujumbe huo katika mkutano na wanahabari Jijini DSM, Zitto amesema kuwa yeye na chama chake wameamua kumuandikia barua Rais Magufuli kwakuwa janga hilo ni kubwa, hivyo kuna haja ya kushirikiana kwa pamoja na Serikali.
“Nimemuandikia barua rasmi Rais Magufuli kuhusiana na mapendekezo yangu na ya chama changu cha ACT wazalendo juu ya namna bora ya kudhibiti na kukabiliana na virusi vya Corona hapa nchini” Zitto.
“Rais na Serikali yake wametangaza hatua za kupunguza kasi ya virusi hivi zikiwemo wananchi kujizuia na mikusanyiko isiyo ya lazima, kunawa mikono kwa maji safi yanayotiririka na sabuni pamoja na kuundwa kwa kamati 3 za baraza la mawaziri kuratibu mpango mzima. Hatua hizi ni za kupongezwa” Zitto
HAWA NI WATU MAARUFU DUNIANI WALIOPATA CORONA, MKE NA MUME, MWANAMFALME, WAZIRI MKUU