Waziri wa kilimo Hussein Bashe ameitaka bodi ya sukari kushirikiana na tume ya taifa ya umwagiliaji kuainisha maeno ya mashamba na kufanya vipimo ili kuwekeza kwenye kilimo cha umwagiliaji kutokana na asilimia kubwa ya wakulima utegemea kilimo cha Mvua.
Waziri Bashe ameyasema wakati wa kongamano la kumi la wadau wa sukari mkoani Morogoro ambapo amewaagiza Taasisi ya kilimo TARI kuanzisha mashamba ya kuzalisha mbegu ya miwa ili kuongeza tija katika zao hilo.
Waziri Bashe amewakikishia wawekesaji kuliznda uwekezaji wao katikia uzalishaji wa sukari ili kuondokana na changamoto mbalimbali ambazo zimekuwa zikirudisha nyuma.