Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Innocent Bashungwa amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Amos Makalla kukutana na Wadau na Wamiliki wa Maabsi ili kuweka utaratibu mzuri ambao ni shirikishi wa utoaji huduma kwa Wananchu kwenye kituo kikuu cha mabasi cha Magufuli Dar es salaam.
BashuNgwa ametoa maelekezo hayo leo Agosti, 30, 2022 wakati akitoa ufafanuzi kuhusu malalamiko ya utoaji wa huduma kwa Wananchi wanaoingia Mkoa wa Dar es salaam kupitia kituo kikuu cha Mabasi cha Magufuli