Baada ya Beyonce kuachia Album yake ya ‘The Lion King: The Gift’ iliyowashirikisha wasanii kibao kutokea Afrika Maghabiri siku kadhaa zilizopita sasa kila mmoja ametoa mawazo yake kuhusiana na wasanii wa Afrika Mashariki kutopewa nafasi kusikika kwenye Album hiyo.
Mastaa mbalimbali kutokea Afrika Mashariki wamejitokeza na kudai kuwa filamu hiyo ya ‘The Lion King’ inazungumzia vitu vingi ambavyo vinapatikana Afrika ya Mashariki na kusema kuwa maneno mengi yaliyotumika ni ya Kiswahili ikiwemo neno kama ‘Simba’ ‘Hakuna Matata’ ‘The Pride of Africa- Serengeti’ ambayo inapatikana Tanzania na pia katika wimbo wa ‘Spirit’ maneno ya kwanza yaliyosikika ni ya Kiswahili.
Mwana- Hip Pop Ay aliingia kwenye Twitter yake na kuandika ‘Nimeona story ya Movie ya Lion King kweli wametukosea Ila tukumbuke tunatengeneza wanamuziki wengi Afrika Mashariki lakini tunafeli kutotengeneza watu wa kufanya kazi kwenye vyombo vya habari vikubwa zinazopitisha maamuzi makubwa, hiyo njia tunaishahau sana na tukiendelea hivyo tutasibiri sana’
Mtangazaji kutokea idara ya BBC London Salim Kikeke aliandika mawazo yake kuhusiana na hilo kwenye ukurasa wake wa instagram
“Mpendwa Beyonce, Mimi ni mpenzi mkubwa wa kazi zako, Nimeona wasanii uliowachagua kwenye Album yako mpya ya The Gift, Nimefadhaika kutoona hata msanii mmoja kutoka Africa Mashariki hasa Tanzania, Filamu yako ya The Lion King imesetiwa na fahari ya bara la Africa kama Serengeti ambayo ipo Tanzania, neno la hakuna matata na Simba ni maneno ya Kiswahili ambayo yanatumika Tanzania na Africa Mashariki.”
“Kuna baadhi ya maneno ya Kiswahili umetumia kwenye wimbo wako wa Spirit, na hawezi kupata maana halisi Kiswahili kwa kuweka wasanii ambao wanatokea Afrika Magharibi peke yake, haijalishi wana uzuri kiasi gani, hata Tanzania na Afrika Mashariki kuna wasanii wenye vipaji ambao wangekuwepo kwenye hiyo kazi yako mpya”
DC wa Kisarawe Jokate Mwegelo hakutaka hili limpite hivyo akaamua kuandika mawazo yake na kusema kuwa alitamani wasanii wa Afrika Mashariki wangeshirikishwa.
“Beyonce kwenye Album na waimbaji wazuri kutokea Afrika,Natamani angeshirikisha na msanii/wasanii kutoka Afrika Mashariki tungesikia na Kiswahili, Hakuna Matata 😕 @beyonce #TheLionKing 🦁 #HakunaMatata“
PART II: ZARI AONGELEA NDOA YAKE SOUTH AFRICA, KUACHANA NA DIAMOND