March 29, 2017 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dr. Harrison Mwakyembe alifanya mkutano na Waandishi wa Habari Dodoma na kuzungumzia mikakati ya Wizara yake.
Moja ya swali aliloulizwa na wanahabari ni kuhusu ripoti iliyoachwa na Waziri wa zamani wa Wizara hiyo Nape Nnauye kuhusu uchunguzi wa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda kudaiwa kuvamia ofisi za Clouds Media huku akiwa na askari wenye silaha.
‘Wengi mnauliza nimeifanyia kazi gani ripoti ya Nape. Mimi hiyo ripoti sijaiona na kama Mwanasheria kwangu ni mwiko na sitapeleka taarifa ambayo haijakamilika’ – Waziri Mwakyembe.
‘Kupitia vyombo vya habari taarifa imeeleza kuwa ushahidi ulitolewa na upande wa Clouds Media na mkakiri kuwa upande wa pili haukupatikana’ – Waziri Mwakyembe.
‘Huwezi kuwa Hakimu kwenye suala lako wewe mwenyewe. Kufanya hivyo ni ubatili, kwa hiyo hata mimi ningekuwa ni Mwandishi wa Habari ningesema hili jambo siliwezi kwa kuwa linanihusu na mimi.’ – Waziri Mwakyembe.
‘Kanuni zinataka kusikiliza upande wa pili, sasa mmeshasema kitu kina upande mmoja halafu nimpelekee kiongozi wangu…NO. Mimi kazi yangu ni kupata maelezo ya upande wa pili na nitapata.’ – Waziri Mwakyembe.
‘Hili jambo ni la kufa na kupona, yaani niache kukutana na wakuu wa Idara mbalimbali hapa kuhakikisha nakuza suala la sanaa na kuhakikisha vijana wetu hawaendelei kuibiwa nibaki kuhangaikia suala la ripoti.’ – Waziri Mwakyembe.
‘Mimi sikuapa kwa jambo hilo moja pekee, lakini mimi ni Mwanasheria mkongwe na nitahakikisha nalifuatilia lakini mimi sitaunda Kamati katika jambo hilo.’ – Waziri Mwakyembe.
‘Lengo letu ni kuhakikisha hatutakuwa na matukio ya namna hiyo katika safari, lakini tukitoka na kauli za papara tutakuwa tunajitafutia matatizo hapo mbeleni. ’ – Waziri Mwakyembe.
Full video wakati Waziri Mwakyembe akijibu maswali nimekuwekea tayari hapa chini….
FULLVIDEO: Alichoongea Nay wa Mitego baada ya kuachiwa na polisi
BREAKING NEWS zote na stori za mastaa utazipata kwa Reporter wako MillardAyo, hakikisha umejiunga na mimi kwenye Facebook, Twitter, Instagram, Snapchat, Youtube, APP kwenye ANDROID na IOS kote huko kwa jina hilohilo la @millardayo