Burudani

Ben Pol kufunga mwaka 2020 kwa ngoma mpya kila wiki

on

Msanii wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul ‘Ben Pol’ ameshukuru mashabiki kwa Kumpa ushirikiano kila anapotoa nyimbo yake mpya, huku akiwataka waupokee wimbo wake mpya unaoitwa Hiyo ndio Mbaya.

Ben Pol amekuwa akipata ushirikiano mkubwa hivyo ujio wa wimbo wake huo mpya aliutoa kwa staili ya Singeli ameshukuru kwa kuwa na na mapokeo makubwa.

“Nashukuru kwa support ninayopata kutoka kwa mashabiki zangu na wadau , sasa nina miaka 10 kwenye muziki wamekuwa na mimi bega kwa bega, sasa nimekuja na wimbo singeli unaitwa “Hiyo ndio Mbaya” ambao nimemshirikisha msanii mpya Tamimu”

”studio tumefanyia Pizzey Records, Producer ni Jay Stereo, katika kufunga mwaka nitatoa wimbo mpya kila wiki, mashabiki zangu wajiandae kupokea kazi zangu’alisema Pol”

“Pia nimeanza kuzunguka mikoani kufanya matamasha ya kuwashukuru mashabiki zangu nimeanzia Mbeya , mikoa mingine inafuata naomba wanipokee”

Soma na hizi

Tupia Comments