Usiku wa December 2 kuamkia December 3 ulipigwa mchezo wa Copa del Rey ambapo klabu ya Real Madrid ya Hispania ilikuwa mgeni wa klabu ya Cadiz na kufanikiwa kuibuka na ushindi wa magoli 3-1, awali Real Madrid ilikuwa inahusishwa kutolewa katika michuano hiyo licha ya kuwa iliibuka na ushindi wa goli 3-1.
Stori za Real Madrid kutolewa katika mashindano hayo zilianza baada ya mchezo kumalizika na kugundua kuwa kocha wa Real Madrid Rafael Benitez alimpanga Denis Cheryshev ambaye hakustahili kucheza mchezo huo kutokana na kuoneshwa kadi tatu za njano katika mashindano yaliyopita.
Denis Cheryshev ambaye ni winga wa kimataifa wa Urusi mwenye umri wa miaka 24 alionyeshwa kadi tatu za njano, wakati akiwa na kwa mkopo katika klabu ya Villarreal msimu uliyopita. Denis Cheryshev ambaye amesababisha Real Madrid kutolewa katika Kombe la Copa del Rey alikuwa staa wa kwanza kufunga katika ushindi wa goli 3-1 dhidi ya Cadiz usiku wa December 2.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.