Benki Kuu ya Tanzania imetoa taarifa ya kuwa noti za Tanzania zimeundwa kwa namna ambayo zinaweza kuzuia vimelea kusalia kwenye noti hizo.
Hata hivyo, kwa kutambua kuwa noti hupita kwenye mikono ya watu wengi, benki kuu imeshauri watumiaji wa noti hizo kunawa mikono mara baada ya kushika noti hizo.
“Noti zetu zimetengenezwa kwa namna ambayo zinaweza kuzuia vimelea kusalia kwenye noti, hata hivyo kwa kuwa noti hizo zinapita katika mikono mingi, tunawashauri Wananchi kuzingatia miongozo ya kunawa mikono mara kwa mara kwa kutumia maji yanayotiririka na sabuni au sanitizer”-Benki Kuu ya Tanzania (BOT)
“Katika kipindi hiki ambacho tuna janga la corona, tunawashauri Wananchi kufanya miamala kwa kutumia njia mbadala za malipo kama simu za mkononi, intaneti na kadi bila kulazimika kufika kwenye kaunta za benki au ATM kuchukua noti”-BOT
“Corona ni tishio Duniani kote na tayari Tanzania tuna wagonjwa watatu, tunawasihi Wananchi katika kipindi hiki ambacho Taifa linapambana na corona kuzipuuza taarifa zinazozagaa mitandaoni ambazo hazina vyanzo vya uhakika, zinazozihusisha noti zetu na usambazaji wa corona” – BOT
KUJIKINGA NA CORONA ZURII NA MALOJI WATOA MSAADA HOSPITALI YA MUHIMBILI NA STAND YA DALADALA