Leo September 14 2016 Gavana wa benki wa Benki kuu ya Tanzania Prof. Benno Ndulu ameitoa taarifa kuhusu hali ya uchumi kati ya mambo aliyoyazungumza ni pamoja na kuhusu hali ya hazina ya fedha za kigeni nchini.
Prof. Ndulu amesema hazina ya fedha za kigeni imeendelea kuwa ya kuridhisha na kuendelea kukidhi mahitaji ya fedha za kigeni kwa ajili ya kuagiza bidhaa na huduma nje ya nchi, ikiwa ni pamoja na kuongeza imani kwa wawekezaji katika uchumi japo kumekuwepo na ucheleweshwaji wa fedha za wahisani na mikopo ya kibiashara kutoka nje ya nchi.
Aidha ameongeza kuwa hadi mwezi June 2016, akiba ya fedha za kigeni ilifikia dola za Kimarekani milioni 3,870.3 ambazo zinatosheleza kuagiza bidhaa na huduma kutoka nje ya nchi kwa takriban miezi 4. Wakati huo huo, rasilimali za fedha za kigeni za mabenki zilikuwa kiasi cha dola za Kimarekani milioni 835.0.
Unaweza kuangalia video hii hapa chini
ULIKOSA UFAFANUZI ULIOTOLEWA NA BOT KAMA SHILINGI IMEPANDA THAMANI AU IMESHUKA? UNAWEZA KUANGALIA VIDEO HAPA CHINI