Kulikuwa na story mitandaoni ambazo hazikuwa nzuri kwa familia ya mzee Mathew Knowles, ikasemekana eti amefilisika mpaka kafikia hatua ya kuuza vitu mbalimbali ikiwemo nguo za mtoto wake, yaani Beyonce pamoja na CD za nyimbo.
Hii haikuwa taarifa nzuri, Beyonce kaongoza kwa kuingiza pesa nyingi upande wa mastaa wa kike Marekani, ina maana amemtelekeza Baba yake kiasi hicho?
Mzee Knowles amekanusha story hizo; “Ningehitaji pesa nisingeuza T-shirt ya dola 5, ningeuza tuzo ya Grammy au BET…“
Mzee huyo kasema anauza vitu hivyo ili kupunguza mlundikano wa vitu ambavyo vilikuwa vinajaza nafasi tu ndani ya jengo la ofisi yake ambayo anapanga kuikarabati upya mwaka 2015.
Kwa hesabu ya haraka haraka ya vitu anavyoviuza Mzee Knowles ni kama atapata dola 2000/= tu.
Hayo yanaendelea Marekani, lakini Beyonce yuko na familia yake, Jay Z na mtoto wao Blue Ivy maeneo ya Thailand, picha za mwisho wameshare wakiwa kwenye ukumbi mkubwa wa Michezo wa Muay Thai wakiangalia mchezo wa ngumi.
Hapa kuna video inayoonyesha Mzee Knowles akiendelea na mauzo ya vitu hivyo.
Nakuhakikishia kwamba nitakufikishia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>>twitter Insta Facebook