Taarifa kutoka nchini Italia zinadai, mwanamke mmoja mwenye umri wa miaka 104, ameweka rekodi mpya ya kupata maendeleo mazuri ya kiafya baada ya kupambana na ugonjwa unaosabbaishwa na Virusi vya Corona.
Mzee huyo aitwaye Ada Zanusso alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa unaosababishwa na Virusi vya Corona, amepata nafuu wakati akipatiwa matibabu nyumbani kwake Biella Kaskazini mwa nchi ya Italia.
Akitoa dalili za kuhusu ugonjwa huo mzee huyo amesema alikuwa anatapika, homa, kupata ugumu wa kupumua na alivyofanya vipimo akakutwa na virusi vya Corona.
Daktari aliemtibu “Ameweza kuamka kutoka kitandani wala sio uongo na anaweza kutembea kwenda kwenye kiti chake, kuendelea kwake vizuri ni furaha kwetu na inatupa matumaini kwa wote wanaoumwa kwa wakati huu mgumu“.
Ana Zanusso amevunja rekodi ya Mr. P mwenye miaka 101, kuwa mtu wa kwanza mwenye umri mrefu kupona ugonjwa wa Corona nchini Italia.
Pia mwanamke mwingine ambaye jina lake limehifadhiwa kutoka nchini Iran mwenye miaka 103, naye amepona Corona baada ya kuumwa kwa siku tatu.