Rais Joe Biden wa Marekani amesaini amri inayolenga kulinda haki ya kutoa mimba, uamuzi huo ni kujibu uamuzi wa hivi karibuni wa Mahakama ya Juu kufuta haki ya kikatiba ya kutoa mimba nchini humo.
Amri hiyo inawataka Maafisa wa afya kuzingatia kuruhusu fedha za umma kutumika kuwasaidia Wanawake kusafiri kwenda kwenye majimbo wanakoweza kutoa mimba.
Hata hivyo, hatua hiyo inatazamiwa kuwa na mafanikio madogo, kwani wajumbe wa Republican wanapigania kuwepo kwa sheria za kuzuia utoaji mimba kwenye majimbo kadhaa ya Marekani.
Uamuzi wa Biden unafanyika siku moja tu baada ya wapigakura wa Kansas kukataa kuondoa ulinzi wa kutowa mimba kwenye katiba ya jimbo hilo, Kura hiyo lilikuwa jaribio la kwanza tangu uamuzi wa Mahakama ya Juu.
Biden ameiita kura hiyo kuwa ushindi na onyo la wazi kwa wanasiasa wanaoingilia haki za wanawake, amesema Mahaama ya Juu na Republican hawajui chochote kuhusu nguvu ya Wanawake wa Marekani.