Waziri wa Madini Dotto Biteko amemvua madaraka Mwenyekiti wa Soko la Madini Chunya, pamoja na kuwasimamisha kazi wafanyakazi wengine watatu.
Biteko amefanya maamuzi hayo leo alipotembelea soko hilo katika ziara yake anayoendelea nayo, ikiwa ni siku chache tangu ateuliwe na kuapishwa kuitumikia Wizara hiyo, ambapo amesema Mwenyekiti huyo amekuwa na uzembe kiasi cha madini kutoroshwa.
Aidha Waziri Biteko pia amefuta leseni za wachimbaji watano ambao wamevunja taratibu mbalimbali pamoja na ameagiza mawakala na wanunuzi wa dhahabu watatu kukamatwa kwaajili ya kuchukuliwa hatua.
Kwa upande wake Mkuu wa mkoa wa Mbeya Albert Chalamila amemwagiza RPC kuwakamata wahusika wote na kuwafikisha kwenye mkono wa sheria mara moja.