Ni siku moja tangu mchekesheji Eric Omondi kutoka Kenya kuachia video ya cover ya wimbo wa Sauti Sol, ‘Kuliko Jana’ kama ambavyo imekuwa kawaida yake kufanya cover za nyimbo zilizo trend za baadhi ya wasanii. Msanii Baraka the Prince kupitia ukurasa wake wa Instagram amesema hajapendezwa na kitendo cha Eric Omondi kutumia uhusika aliovaa katika video hiyo kwani haipendezi katika maadili ya imani ya wakristo na imemchukiza.
Unaweza kutazama video iliyofanywa na Eric Omondi ambayo Baraka anasema haijamfurahisha>>>