Shirika la viwango Tanzania [TBS], leo April 29,2021 limetoa mafunzo kwa wadau wa mchele Mji mdogo wa Katoro Wilayani Geita.
Akitoa mafunzo hayo kwa washiriki Meneja kutoka TBS Kanda ya Ziwa Mhandisi Joseph Ismail Mwaipaja ametoa elimu kwa wadau hao huku akiwataka kuzingatia Viwango kabla ya kuzipeleka sokoni bidhaa zao.
Aidha Mhandisi Mwaipaja amewafundisha washiriki majukumu ya TBS ikiwa ni pamoja na kuwaeleza huduma zinazotolewa na namna gani wao kama wadau wanaweza wakafaidika na kuleta tija kwa biashara zao.
Kwa upande wao baadhi ya washiriki waliopata mafunzo hayo wamesema mafunzo hayo yana tija kwao na yamekuja wakati muafaka hususani katika kipindi hiki cha msimu wa Mavuno ya mpunga huku wakiishukuru serikali kwa kuona umuhimu wa kupata mafunzo kwani yatawasaidia kuthibitisha ubora wa bidhaa zao na hatimaye kuuza mazao yao nje ya nchi.
KIJANA ALIEANZA KUPAKA RANGI HADI KUMILIKI KAMPUNI NA KUAJIRI “NILIACHA MZIKI, NKAWA FUNDI TILES”