Wakati uchaguzi mkuu wa Shirikisho la soka duniani FIFA ukitarajiwa kufanyika kesho mjini Zurich Uswiss, Rais anayewania nafasi hiyo kwa mara nyingine Sepp Blatter amekataa kujiuzulu nafasi hiyo.
Blatter ameshinikizwa kujiuzulu baada ya shirikisho hilo kukumbwa na kashfa ya rushwa ambapo tayari Maafisa saba wa FIFA wakishikiliwa kwa tuhuma za rushwa.
Rais wa Shirikisho la soka Ulaya, Michael Platini amesema Blatter amekataa kujiuzulu na uchaguzi wa FIFA utafanyika kama ulivyopangwa.
Platini amesema UEFA itashiriki uchaguzi huo kesho na imewashauri washirika wake kumpigia kura mpinzani wa Blatter ambaye ni Ali-Hussein kutoka Jordan.
Afrika pamoja an Asia wameahidi kumpigia kura Blatter.
Unahitaji chochote ninachokipata kisikupite? jiunge na mimi kwenye Twitter, Facebook na Instagram kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.