March 15 2016 kituo cha ITV kiliripoti taarifa kutoka visiwani Zanzibar ambapo ilidaiwa kuwa na taarifa za watu wasiojulikana kurusha bomu nyumbani kwa Kamishna wa jeshi la polisi Visiwani Zanzibar eneo la Kijichi.
Sasa taarifa niliyoipata ni kwamba nyumba ya Kamishna wa Jeshi la Polisi Zanzibar Hamdani Omar Makame imelipuliwa na kitu kinachosadikiwa kuwa ni bomu na watu wasiojulikana majira ya saa 5.00 usiku huko Kijichi nje kidogo ya mji wa Zanzibar.
Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari Ofisini kwake Makao Makuu ya Polisi Kilimani, Kamishna Hamdani amesema tukio hilo limeathiri sehemu ya paa la nyumba na dari na kujeruhi baadhi ya watu waliokuwa wamelala na kusababisha hasara kubwa.
Amesema tukio hilo linafanana lile lililotokea tarehe 03 mwezi huu katika Maskani ya CCM Kisonge Unguja hivyo polisi inaendelea kufanya uchunguzi ikiwa ni pamoja na kuwasaka wahalifu wanaofanya uhalifu huo.
Akizungumzia matukio mengine ya uhalifu na kuchoma moto nyumba, maskani na kituo cha Afya huko Pemba, alisema Jeshi la Polisi limeanza msako mkali na kuwatia mbaroni watu 31 ambao wanaendelea kuhojiwa na watakaohusika watafikishwa katika vyombo vya sheria.
Kamishna Hamdani amewatoa hofu wananchi kuhusu usalama wao na mali zao kuelekea uchaguzi wa marudio utakaofanyika tarehe 20 mwezi huu na kuwepo kwa ongezeko la askari katika maeneo mengi ya mijini na vijijini ni moja ya juhudi za kuimarisha ulinzi na kuhakikisha uchaguzi huo utakuwa salama na amani.
Source:Full Shangwe
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line yatiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter,FB,InstagramnaYouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FBYOUTUBE
ULIKOSA HII YA CHEGE KAONGELEA: KILCHOTOKEA KWAKE NA JUMA NATURE MWAKA JANA, UGOMVI WA UHURU NA SWEETY SWEETY