Vikao Vya bunge la 11 vimeendelea tena leo April 20 2016, mambo mbalimbali yamejadiliwa ikiwa ni pamoja hii ishu ya mauaji ya vikongwe nchini, swali lililoulizwa na Mbunge wa viti maalum Tauhida Cassian amesema ‘Je, Serikali ina mkakati gani wa kunusuru mauaji ya vikongwe nchini?’
Jibu likatolewa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Hamad Masauni ‘Serikali kupitia jeshi la Polisi imeweka mikakati mbalimbali ya kunusuru mauaji ya vikongwe nchini ikiwa ni pamoja na 1. Kufanya oparesheni na misako ya mara kwa mara kubaini waganga wa jadi wanaojihusisha na upigaji ramli na wasiofuata taratibu za kisheria’
‘’2. Kutoa elimu kupitia Polisi jamii, wadau mbalimbali wa ulinzi na usalama, 3. Kuanzishwa kwa vikosi kazi ili kuwezesha kufuatilia na kutafuta taarifa za watuhumiwa’
‘Pia naomba nitumie fursa hii kutoa rai kwa Wananchi kuacha vitendo vya kujichukulia sharia mkononi na kusababisha mauaji’
Jambo lingine lililopata nafasi ya kuzungumziwa ni hii ya changamoto za wavuvi, Hamad Salim Maalim aliuliza ‘Je, Serikali imejipanga kwa kiasi gani kuwasaidia wavuvi wadogowaogo Tanzania kusaidia maendeleo ya taifa na kujikwamua na umaskini?’
Naibu Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi William Nasha akasema ‘Serikali inatekeleza miradi mbalimbali ikiwemo mradi wa maendeleo na usimamizi shirikishi wa uvuvi, mradi umelenga kuboresha utawala bora kwenye jamii za wavuvi, kusaidia mitaji, elimu na kuboresha miundombinu’
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE
Ilikupita hii Video ya Yaliyotokea bungeni Dodoma April 19 ?