Leo May 2, 2018 Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu inatarajia kusikiliza kwa siku 2 mfululizo ushahidi wa kesi inayomkabili Ofisa Msaidizi wa Forodha wa (TRA), Jennifer Mushi anayedaiwa kumiliki magari 19 yenye thamani ya Shilingi Milioni 197.6 yasiyolingana na kipato chake.
Hayo yameelezwa mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi baada ya Mwendesha Mashtaka wa Jamhuri, Inspekta Hamis kueleza kuwa shauri hilo limeitishwa kwa ajili ya kusikilizwa.
Hata hivyo, Inspekta Hamis amedai kuwa hana taarifa za kutosha kuhusu usikilizwaji wa shauri hilo kwani lipo chini ya Mawakili wa TAKUKURU na hawapo mahakamani.
Baada ya kueleza hayo Hakimu Shaidi ameahirisha kesi hiyo hadi May 28 na 29, 2018, kwa ajili ya kuanza kusikilizwa mfululizo.
Katika kesi hiyo, mshtakiwa anadaiwa kati ya March 21, 2016 na June 30, 2016 maeneo tofauti ya Jiji la Dar es Salaam, akiwa mfanyakazi wa TRA alikutwa akimiliki mali zisizolingana na kipato chake, kinyume na sheria.
Inadaiwa alikutwa akimiliki magari 19, yakiwemo Toyota Ra4,Toyota dyna truck, Toyota viz, Suzuki carry na Toyota Ipsum yote yakiwa na thamani ya Mil.197,601,207
Pia anadaiwa kati ya March 21, 2012 na March 30, 2016 maeneo ya Dar es salaam akiwa muajiriwa wa TRA aliishi maisha ya kipato cha juu (kifahari) tofauti na kipato chake yenye thamani ya Sh.Mil 333.2
MAGAZETI LIVE: Maumivu, Vyeti feki bado mtihani mzito, Kanisa lazuia shela maharusi wajawazito