Msemaji wa familia ya kijana aliyeuawa na polisi Tarime Mbunge John Heche amesema Polisi aliyehusika na kifo cha Suguta Chacha ametiwa hatiani na kupandishwa kizimbani na kusomewa shtaka la mauaji.
Kufuatia hatua hiyo Familia ya Marehemu imesema baada ya kufanya mashauriano ya muda mrefu familia imekubali kumzika ndugu yao ambapo mazishi yatafanyika Alhamisi ya May 3, 2018 kijiji cha Nyabitocho mara baada ya familia kuridhika hatua zilizochukuliwa dhidi ya mtuhumiwa.
Hivyo familia imekubali kuchukua mwili huo na tayari kwa kuuzika, Heche alitumia kurasa zake za mitandao ya kijamii kutoa taarifa hiyo kwa umma.
”Tumeridhika na hatua zilizochukuliwa na polisi kwa kumtia hatiani mtuhumiwa kumfikisha mahakamani na kusomewa shtaka la kuua, kama familia tumeona ni vyema tuutangazie umma kuwa kesho tutauchukua mwili wa marehemu na kuuleta nyumbani na kesho kutwa (Alhamisi May 3) tutamzika” amesema Heche.
MAGAZETI LIVE: Maumivu, Vyeti feki bado mtihani mzito, Kanisa lazuia shela maharusi wajawazito