Ni muda mrefu kumekuwa na malalamiko ya wanawake kupata mimba wakiwa wanatumikia vifungo gerezani, siku ya leo katika kikao cha bunge Dodoma swali lililoulizwa ni kuwa wahusika wa mimba hizo ni akina nani wakati wafungwa hawana ruhusa ya kuonana na wapenzi wao?
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani alianza kujibu swali hilo, “.. Hatuna utaratibu wa kisheria hapa nchini unaoruhusu wafungwa kukutana faragha na waume au wake zao kama baadhi ya waheshimiwa walivyoomba.. Jeshi la magereza linao utaratibu wa kuwatenganisha wafungwa wa aina zote wanapiokuwa magerezani.. Wafungwa wa kiume hutunzwa selo zao wkati wafungwa wa kike huwa na gereza lao ambalo hulindwa na askari wa aina yao.. Hakuna uwezekano wa wafungwa au askari wa kiume wanaoweza kuingia kwenye sehemu ya wanawake.. Sio rahisi mfungwa wa kike kupata ujauzito akiwa gerezani.. Ujauzito unaoonekana magerezani huwa unaanzia nje yaani uraiani..”- Pereira Silima.
Baada ya majibu hayo Mbunge wa Viti Maalum CUF, Rukia Ramadhani hakuonyeshwa kuridhishwa na majibu hayo na kuuliza kuhusu kesi za ulawiti; “.. Kwa kuwa katika jibu lake la msingi amesema kwamba katika magereza yetu hakuna mwanya wa kupatikana vitendo vya kujamiiana.. Hawa mashehe waliokamatwa Zanzibar wakaletwa bara ambao wanalawitiwa jambo ambalo ni laana kwa Mungu na ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu inatokea vipi? Ni kawaida wafungwa wanatolewa nje kufanya shughuli za usafi, kulima pamoja na mambo mengine na pia wengine hupelekwa katika nyumba za maafisa magereza kufanya usafi na kupika. Haoni kama faragha hii inatosha kutokezea hili nililomwambia..?”
Akijibu swali hilo Waziri wa Mambo ya Ndani amesema; “.. Mmoja katika wahitakiwa hawa anaitwa Sheikh Salum Ally Salum a.k.a yake anaitwa ‘Al Qaeda’.. Huyu ndiyo aliyelalamika kwamba ametendewa vitendo visivyokuwa sahihi akiwa Polisi.. Kwa malalamiko yake sio gerezani, akiwa katika mikono ya Polisi.. Toka akamatwe ameshafika Mahakamani zaidi ya mara tatu, lakini ya nne ndiyo akaenda kulalamika.. Sasa malalamiko hayo na sisi yanatushangaza kwa hiyo ndiyo tunayachunguza.. Tulichofanya kitu cha kwanza tumempeleka Hospitali Amana na kesho tarehe 13 atakwenda Hospitali Muhimbili kuchunguzwa.. lakini na sisi tunachunguza pia kuhusu tabia zake za nyuma kabla hajaja.. kabla hajaingia katika mgogoro na sheria.. kwa hiyo tukishapata taarifa hizo tutajua hatua za kuchukua..”-Mathias Chikawe.
Kusikiliza sauti za maswali na majibu hayo kutoka Bungeni leo bonyeza play hapa.
Una comment yoyote mtu wangu wa nguvu, unaweza kuiweka hapa na pia ku-share stori hii na mwenzako.