TZA ina ripota nchini Kenya aitwae Julius Kipkoich ambae amekua na mfululizo wa ripoti mbalimbali za Kenya kupitia Amplifaya ya Clouds FM lakini pia kwenye millardayo.com na AyoTV.
Kipkoich alitembelea maduka 10 maarufu ya kuuza movie mjini Nairobi na kuulizia kama kuna movie yoyote kutoka Tanzania lakini alijibiwa hakuna na kwamba movie za Tanzania haziuzwi wala kuagizwa na wauzaji Nairobi.
Sababu ni chama cha kutoa haki miliki kwa muziki na movies kenya (MCSK) kinachukulia movie za kitanzania kama za Kenya hivyo haziruhusiwi kuuzwa na mtu asie na kibali kutoka kwao.
Kwa wale wachache walio na kibali wanasema movie nyingi kutoka Tanzania zikiagizwa huwa zinauzwa sana Mombasa na maeneo mengine ya Pwani mwa Kenya kwa sababu wengi wanaoishi maeneo hayo wanapenda kuzitazama movie za kiswahili hasa za Tanzania.
Unaambiwa kwa sasa Mombasa ndio sehemu inayoongoza sana pia kwa kucheza sana muziki wa bongofleva kuanzia kwenye sehemu za starehe mpaka kwenye redio na ndio maana wasanii wengi wa bongofleva pia hupata shows nyingi huko kuliko sehemu yoyote nyingine ya Kenya.
Kuna upande wa pili wa hii stori hivyo endelea kukaa karibu na millardayo.com kupitia twitter instagram na facebook kwa jina hilohilo la @millardayo nikipata chochote kingine nitakutumia link moja kwa moja mtu wangu