AyoTV

Sababu za Mkomola kuanzishiwa benchi Serengeti Boys vs Niger (+video)

on

Usiku wa leo May 21 2017 timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17 Serengeti Boys itacheza mchezo wake wa mwisho wa Kundi B dhidi ya timu ya taifa ya Nigerkwenye uwanja wa Port Gentil uliyopo kisiwani ndani ya nchi ya Gabon.

Kocha wa Serengeti Boys Bakari Shime ameongea na Waandishi kabla ya game hiyo ambayo amefanya mabadiliko ya kumuanzishia benchi Yohana Mkomola na kumuweka aanze Ibrahim Ally kwenye kikosi cha kwanza.

“Vijana wana ari ya kutosha japo tunaamini utakua mchezo mgumu, ni mchezo mmoja tu wa kuamua kama tutabaki kwenye mashindano au tutaondoka, mabadiliko kidogo yapo ni mchezaji mmoja tu ambaye mashindano haya hajacheza Ibrahim Ally ambaye ataongoza mashambulizi badala ya Yohana Mkomola ambae yuko salama na tutamtumia baadae Bakari Shime

Kumtazama zaidi kocha akiongea bonyeza play hapa chini kumsikiliza na mengine atakayosema

ULIPITWA? Hii video hapa chini ina maelezo yote ya Alfred Lucas kuhusu Issa Makamba wa Serengeti Boys kurudishwa Tanzania

Soma na hizi

Tupia Comments