Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje, Bernad Membe ametinga Mahakama Kuu ya Tanzania kwa ajili ya kusikiliza mwenendo wa kesi yake dhidi ya Cyprian Musiba.
Akizungumza na waandishi wa habari, Wakili wa Membe, Jonathan Mndeme amesema shauri la mteja wake ni 220 ya mwaka 2018.
Amesema shauri hilo limeitishwa mbele ya Jaji Luvanda ambapo hadi leo hawajapokea majibu ya Musiba na wenzake wawili kuhusu madai yanayowakabili.
Ameeleza kuwa Mawakili wa Musiba wameiomba mahakama muda wa kujibu madai hayo uongozwe ambapo Jaji amewakubali na amepanga Mei 17, 2019 kuyasikiliza.
BREAKING: KESI YA BERNAD MEMBE NA MUSIBA, MAHAKAMA KUU IMEYAPANGA HAYA