Klabu ya Azam FC imeanza rasmi maandalizi ya kutetea ubingwa wao msimu ujao na michuano ya kimataifa kwa kukamilisha usajili wa mchezaji wa kimataifa wa Burundi aliyekuwa anakipiga kwenye klabu ya Yanga.
Taarifa rasmi zilizothibitishwa na meneja wa Azam FC Jemedari Said ni kwamba mshambuliaji Didier Kavumbagu amejiunga na klabu hiyo kwa mkataba wa mwaka mmoja.
“Ni kweli Kavumbagu tumemalizana nae na amesaini mkataba wa mwaka mmoja. Taarifa zaidi zitatolewa baadae.” Alikaririwa Jemedari.
Kavumbagu alitua nchini Tanzania akitokea Burundi alipokuwa anaitumikia Vital O na kuja kujiunga na Yanga misimu miwili iliyopita.