Leo September 14, 2020 Wanafunzi 10 wamekufa kwenye ajali ya moto iliyotokea katika shule ya msingi Islamic Byamungu iliyopo Wilayani Kyerwa ambapo pia wanafunzi wawili bado hawajapatikana mpaka sasa.
Bweni lililoungua ni la wanafunzi wa kiume ambapo majeruhi 6 wamepelekwa Hospital ya Nyakahanga, akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Mkuu wa Wilaya ya kyerwa “Bweni limeungua usiku huu wa kuamkia leo,chanzo bado hakijajulikana,wamefariki 10 na 6 wamekimbizwa Hospitali”.