Mapenzi ya Chris Brown na mpenzi wake Karrueche Tran sasa yanaonekana kukua na kuimarika kadri siku zinavyokwenda na sasa hata akili zao huenda zikafika mbali na kufikiria hata kufunga ndoa.
Jana ilikua siku ya wapendanao duniani na kila mtu kwa namna yake aliweza kusherehekea na watu au mtu ampendaye kwa namna alivyotaka kufanya.
Kwa upande wa Chris Brown alimwandikia mpenzi wake Karruaeche ujumbe wa kuonyesha anampenda huku akimshukuru kwa kuonyesha kumjali zaidi.
“Happy Valentine’s Day beautiful…. I’m so thankful to have [a] soul that cares for me the way you do. Love you babe”
Kwa upande wa Karrueche ambaye alikua katika mji wa Florida akiandaa filamu naye aliandika ujumbe uliosomeka “Happy Valentine’s Day to my love.. You drive me crazy and you’ve made me crazy but that’s just us I love you just as much as you love trying to match my outfits.
Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia Twitter, Instagram, na Facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>>twitter Insta Facebook