Katikati ya wiki iliyopita wasanii wa Tanzania walipata nafasi ya kupata chakula cha jioni na Mheshimiwa Rais Jakaya Kikwete kwa ajili ya kumuaga na kumshukuru kwenye kipindi cha uongozi wake wa miaka 10 ya uongozi wake kama Rais.
Wasanii walipata nafasi ya kila mmoja kuongea kitu ambacho hawezi kukisahau kwenye uongozi wa Rais Kikwete na ilipofika zamu ya Bushoke aliongea machache ambapo alianza kwa kukumbushia siku ambayo waliitwa na Rais Ikulu kwa ajili ya chakula cha mchana,walipomaliza kula kwa bahati nzuri Bushoke alizipenda sahani pamoja na vijiko vya Ikulu.
Bushoke kwenye sentensi yake ameongea haya pia>>’Wakati tunapakua chakula nikaona sahani zile zina nembo ya ngao ya Taifa,nikazipenda sana zile sahani na vijiko ambavyo navyo vilikua na nembo hiyo hiyo nikaviangalia pale nikasema dah hizi nzuri sana,nikachukulia kitu kidogo sana nikamwambia Mheshimiwa ,Bwana Mheshimiwa samahani na mimi naweza nikapata hizi sahani nikaondoka nazo?Naomba kuondoka nayo nyumbani akanijibu hapana hizo sahani hazinihusu kwa sababu ni sahani za Serikali’.
PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia za siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>> Videos