Yule Justin Bieber ambaye ulikuwa unamjua wakati anatoa album ya My World na wimbo kama Baby, basi sio huyu wa sasa hivi tena.
Kwenye list ya forbes ya over exposed celebrity, Justin Bieber alikaa top kwenye hiyo list kutokana na matukio yake ya kukamatwa na polisi na mengineyo.
Mabadiliko aliyopitia hivi sasa ni kubadilisha muonekano wake kabisa kwa kuchora tatoo kubwa kwenye mikono yake yote miwili.
Bieber ana tatoo kadhaa kwenye mwili wake ambazo zilikuwa hazionekani kutokana na nguo lakini hizi zitakuwa zinaonekana vizuri kwasababu zipo mikononi na rangi yake inaruhusu tatoo kuonekana vizuri.
Kama kawaida ya social media fans wake kwenye instagram kuna waliozipenda na wengine hawajapenda.