Kuendesha gari zuri la kifahari ni moja kati ya ndoto za watu wengi, ila tatizo huja kwenye uwezo wa kununua gari hilo, ambapo kwa wenye nazo si tatizo, wanapata kilicho bora kwa kutumia fedha zao
Kampuni maarufu ya kutengeneza magari ya kifahari zaidi duniani ya Bugatti imekamilisha gari yake ya “La Voiture Noire” lenye thamani zaidi duniani litakalouzwa Dola za Marekani Milioni 18 sawa na Bilioni 41.7 za Kitanzania.
Wataalamu wa magari ya kifahari wanasema gari hilo ndio la gharama kubwa zaidi kuwahi kutengenezwa duniani.
Inaripotiwa kwamba gari hilo jipya limewaacha midomo wazi watu wengi duniani ikiwamo matajiri wenye wenye mapenzi na magari ya kifahari.
Bugatti ni miongoni mwa kampuni kubwa inayosifika kwa kutengeneza gari imara na bora zaidi duniani na kufanya kuwavutia watu wengi wenye uwezo mkubwa kumiliki gari hizi licha ya bei zake kuwa za gharama za juu sana.