Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), linawaita vijana waliohitimu elimu ya sekondari kidato cha sita kwa mwaka 2021, kutoka shule zote za Tanzania Bara kuhudhuria mafunzo ya JKT kwa mujibu wa Sheria.
JKT imewapangia makambi watakayo kwenda kupatiwa mafunzo na wanatakiwa kuripoti makambini kuanzia tarehe 01 hadi 10 June 2021.
Vijana walioitwa wamepangwa katika kambi za JKT Rwamkoma – Mara, JKT Msange – Tabora, JKT Ruvu – Pwani, JKT Mpwapwa, na Makutupora JKT Dodoma, JKT Mafinga – Iringa, JKT Mlale – Ruvuma, JKT Mgambo na JKT Maramba -Tanga, JKT Makuyuni – Arusha, JKT Bulombora, JKT Kanembwa, na JKT Mtabila – Kigoma, JKT Itaka – Songwe, JKT Luwa na JKT Milundikwa – Rukwa, JKT Nachingwea – Lindi na JKT Kibiti- Pwani na Oljoro JKT- Arusha.
Wahitimu wenye ulemavu wa kuonekana kwa macho (Physical disabilities) waripoti katika kambi ya Ruvu JKT iliyopo Mlandizi Mkoani Pwani ambayo ina miundombinu ya kuhudumia watu wa jamii hiyo
Orodha kamili ya majina ya vijana walioitwa, Makambi ya JKT waliyopangiwa na maeneo yaliyopo inapatikana hapo chini.
BONYEZA JINA LA KIKOSI HAPO CHINI KUANGALIA MAJINA YA VIJANA WA MUJIBU WA SHERIA 2021