Siku ya jana Novemba 6, Beyonce alimtembelea Kelly Rowland aliyejifungua mtoto wa kiume na kuacha ujumbe wa nguvu katika ukurasa wake wa Instagram (@beyonce) kwa mtoto huyo.
“.. Hakuna hisia nzuri kama hii ya kumshika mpwa wangu mzuri. Nashukuru Mungu kwa heshima ya kuishuhudia safari ya dada yangu kuwa mama. Nimekuwa nikiota watoto wetu wanakua pamoja. Nashukuru kwa kuungana kwetu. Mtoto Ty, Nakupenda sana. Pongezi kwenu wapenzi..”-Beyonce.
Unapenda stori kama hizi zisikupite? ungana na mtu wako Millard Ayo kwa kubonyeza hapa ili niwe nakutumia moja kwa moja mtu wangu >>> Twitter InstagramFacebook