February 27 klabu ya Dar Es Salaam Young African ilishuka dimbani kumenyana na klabu ya Cercle de Joachim ya Mauritius katika mchezo wake wa pili wa hatua ya kwanza ya michuano ya klabu Bingwa barani Afrika.
Yanga walikuwa katika nafasi nzuri ya kuendelea na hatua inayofuata, baada ya mchezo wa kwanza waliocheza Mauritius kuibuka na ushindi wa goli 1-0, hivyo Cercle de Joachim walikuja kwa nia ya kupata ushindi ili waendelea hatua inayofuata.
Hata hivyo hali haikuwa rahisi kwa Cercle de Joachim kupata matokeo katika mchezo huo, kwani dakika ya 3 Yanga walifanikiwa kupata goli la kwanza kupitia kwa Amissi Tambwe, goli la pili la Yanga lilifungwa na Thabani Kamusoko dakika ya 55 baada ya kutumia vyema mpira wa faulo.
Licha ya kumkosa Donald Ngoma katika mchezo huo, Yanga wamefanikiwa kuibuka na ushindi wa goli 2-0, hivyo watacheza na APR ya Rwanda katika hatua inayofuata na itaanzia kucheza ugenini mjini Kigali mwanzoni mwa mwezi March, na baada ya wiki mbili kurudiana uwanja wa Taifa Dar Es Salaam.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>>INSTAGRAMTWITTERFBYOUTUBE