Raia wa Uingereza jana walikuwa na kazi moja ya kumchagua kiongozi mpya atakayewaongoza kwa muhula mwingine baada ya kufanyika kwa uchaguzi mkuu.
Chama cha Conservatives kilikua na upinzani mkali dhidi ya Labour lakini kura ya Raia hao imeangukia kwa Waziri mkuu wa nchi hiyo David Cameron kushinda kiti cha kuongoza Taifa hilo kubwa duniani kupitia chama chake cha Conservatives.
David Cameron amechaguliwa kwa awamu ya pili na ushindi huo umekuja baada ya kushinda viti 323 alivyohitajika kushinda.
Baada ya kutangazwa kwa matokeo hayo kiongozi wa chama cha Labour cha Uingereza, Ed Miliband amewaambia wanaharakati wa chama hicho kwamba anajiuzulu kama kiongozi wa chama hicho kufuatia matokeo yasiyo ya haki ya uchaguzi huo.
David Cameron anarejea madarakani bila idadi kubwa ya wabunge kwa kuwa Chama cha Conservative kitalazimika kuunda serikali ya muungano.
Miliband amempongeza Waziri mkuu David Cameron kwa kuchaguliwa kwa awamu ya pili na amesema kuwa anachukua jukumu la kushindwa kwa chama chake katika uchaguzi huo.
Unahitaji chochote ninachokipata kisikupite? jiunge na mimi kwenye Twitter, Facebook na Instagram kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.