Michezo

“Cavani nilimuomba asiondoke, nitamtumia” Rangnick

on

Kocha wa mpito wa Manchester United Ralf Rangnick amemuomba mshambuliaji Edinson Cavani kusalia ndani ya viunga vya Old Trafford mpaka mwisho wa msimu huu, huku vilabu vya Juventus na Fc Barcelona vikihusishwa kumnyakua nyota huyo kwenye dirisha dogo la usajili mwezi January 2022.

“Nilimwambia tangu siku ya kwanza, yupo kwenye mipango yangu na namuhitaji kwani yeye ni mchezaji pekee anayeweza kucheza kama mshambuliaji na kulitizama goli la mpinzani kwa hiyo nilimwmbia wazi kwamba namuhitaji abaki nasi na yeye anajua hilo na kwa jinsi gani ninavyompa heshima kubwa’‘ Rangnick

Cavani raia wa Uruguayi ana umri wa miaka 34,alitoka benchi na kuisaidia Manchester United kupata sare ya bao 1-1 dhidi ya Newcastle United na kwenye mchezo uliopita  aliisaidia tena kikosi hicho cha mashetani wekundu kuibuka na ushindi wa magoli 3-1 dhidi ya Burnley huku mkufunzi wa United Ralf Rangnick akiwa na kibarua kizito cha kutoa hatma ya nyota kama Anthony Martial, Jesse Lingard, Donny van de Beek na Paul Pogba.

TIMU YA TAIFA JANG’OMBE IMEJIANDAA KUCHUANA NA YANGA MAPINDUZI CUP, KOCHA AFUNGUKA

Soma na hizi

Tupia Comments